Beki na Nahodha wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Virgil van Dijk amewaambia wachezaji wenzake wana kazi ya kufanya kabla ya msimu mpya haujaanza.

Pia, Beki huyo amewaonya wenzake na kuwataka kuimarika kufuatia kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya FC Bayern Munich katika mechi ya kujiandaa na msimu mpya.

Liverpool ilikuwa ikiongoza 2-0 yaliyowekwa kimiani na Cody Gakpo na Van Dijk. Hata hivyo, Serge Gnabry na Leroy Sane walisawazisha kabla ya Luis Diaz kuongeza bao la tatu matokeo yakawa 3-2.

Aidha Bayern ikapambana na kurudi mchezoni na kufunga mabao mawili ambayo yalipachikwa na Josip Stanisic na Frans Kratzig aliyeweka mpira nyavuni dakika ya 91 ya mtanange huo.

Beki huyo wa Kimataifa wa Uholanzi aliweka wazi kwamba safu ya ulinzi ya Liverpool imekuwa mbovu na imejenga hofu kuelekea msimu mpya wa ligi.

Alichosema cha Televisheni Van Dijk kipitia Kituo cha Liverpool (LFTC): “Kuna mambo mengi tunatakiwa kuyaboresha kabla ya msimu kuanza.

Bayern ni timu nzuri na itakufunga kama utakuwa dhaifu, bado kazi kubwa inatakiwa kufanyika.

Kikosi chetu kina ubora na tulikuwa na uwezo wa kuifunga. Huu ni mwanzo tunachotakiwa ni kujifunza. Mazoezi tunayoyafanya na mechi tunazocheza.”

Mfumo mpya wa Liverpool kuelekea msimu mpya utakuwa wa kushambulia zaidi lakini Washambuliaji wake wana udhaifu kwenye ukabaji akiwemo Darwin Nunez.

Wakati timu inafanya kazi ya kuunganisha wachezaji wapya waliosajiliwa na kuzoea mabadiliko ya kimbinu, wito wa Van Dijk kwa wachezaji wenzake ni kupambana kwa matumaini ya kurudi kwa kishindo msimu huu wa 2023-2024.

Kikosi cha Jurgen Klopp kitacheza mechi ya mwisho ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Darmstadt Jumatatu (Agosti 7) kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea Agosti 13.

Kasi ujenzi wa Mabweni shule ya Sekondari yakataliwa
Ahmed Ally: Hatutaacha kitu 2023/24