Beki kutoka Uholanzi Virgil van Dijk, amechaguliwa nahodha mpya wa Liverpool baada ya Jordan Henderson kutimka katika kikosini.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, alijiunga na Liverpool mwaka 2018 akitokea Southampton, hadi sasa amecheza mechi 222.

Pamoja na Dijk, Trent Alexander-Arnold amechaguliwa kuwa nahodha msaidizi akichukua nafasi ya James Milner aliyejiunga na Brighton.

Henderson na Milner wameondoka katika kikosi cha Kocha Jurgen Klopp, kutokana na kukasirishwa na kiwango kibovu kilichoonyeshwa msimu uliopita, kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Liverpool imeshindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016.

“Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwetu na hakuna aliyekuwa na furaha kutokana na kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

“Hata hivyo hatujakata tamaa ya kuendelea kuitumikia timu hiyo, tunaamini msimu mpya utakuwa mzuri na tutahakikisha tunarudisha heshima ya kubeba mataji,” alisema Van Dijk.

Wachezaji wengine ambao wameondoka Liverpool waliokuwepo wakati wakitwaa ubingwa mwana 2020 ni Naby Keita na Roberto Firmino huku Alex Oxlade-Chamberlain akiwa na matatizo ya majeraha ya muda mrefu.

FCC yaidhinisha maombi miungano ya Kampuni
Uwanja wa Dodoma mbioni kujengwa