Idadi ya wagonjwa wapya wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia 254 baada ya kubainika kwa wagonjwa wapya 83.
Idadi hiyo imeongezeka katika idadi ya 147 iliyotangazwa na Serikali Aprili 17, 2020.
Taarifa iliyotolewa leo, Aprili 20, 2020 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo Aprili 20, 2020 imeeleza kuwa pamoja na kuwapo kwa visa hivyo vipya pia kuna vifo 3 zaidi vilivyotokana na ugonjwa huo.
Wizara ya afya imetoa pole kwa familia walipoteza ndugu zako huku ikisema kuwa wagonjwa wengine wanaendelea vizuri isipokuwa wagonjwa 4 ambao wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi maalumu.
![](https://www.bongoleo.com/wp-content/uploads/2020/04/IMG-20200420-WA0027.jpg)