Naibu Jaji Mkuu Nchini Kenya, Philemona Mwilu amekamatwa jijini Nairobi kwa tuhuma za ufisadi, na kupelekwa makao makuu ya idara ya upelelezi kwaajili ya kuhojiwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, Noordin Haji na mkuu wa idara ya upelelezi, George Kinoti walihudhuria mikutano kadhaa na maafisa wa tume ya huduma ya mahakama kabla ya kukamatwa kwa Mwilu.
Aidha, Gazeti hilo limeandika kuwa mamlaka ya forodha ya Kenya iliripoti kwa idara ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma kuwa jaji huyo alikwepa kulipa kodi ya kiasi kikubwa cha fedha na alihusika katika ubadhirifu wa pesa kupitia benki mbalimbali.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa afisa wa ngazi za juu wa kiwango hicho kutiwa mbaroni kwa tuhuma za ufisadi.
-
Bobi Wine na wenzake waachiwa huru kwa dhamana
-
Video: Ugaidi, Biashara vyateka mkutano wa Trump na Kenyatta
-
Spika wa Bunge atishia kususia vikao
Hata hivyo, Jumatatu wiki hii, vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba jaji mmoja alikuwa akitafutwa na maafisa wa upelelezi kwa tuhuma za ulaji rushwa.