Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amevitaja vita vinavyoendelea nchini Ukraine kama matumizi mabaya ya madaraka yenye nia ya kutimiza malengo binafsi na kuwaweka katika hatari ya machafuko watu wasioweza kujitetea.
Papa Francis amesema hayo katika mkutano wa Kanisa Katoliki katika mji mkuu wa Slovakia, Bratislava, nchi mojawawapo inayopakana na Ukraine ambayo imefungua milango yake kuwapokea wakimbizi.
Russia yakataa kusitisha vita Ukraine
Kiongozi huyo wa kidini hajaitaja Urusi moja kwa moja katika kulaani vita hivyo ila ametumia maneno kama “uvamizi wa kivita usiokubalika” ili kuelezea hoja yake.
Urusi kwa upande wake imesema inachofanya Ukraine ni “operesheni maalum ya kijeshi” ambayo haina nia ya kuiteka nchi hiyo ila kuvunja nguvu ya kijeshi ya jirani yake na kuondoa kile inachokiita unazi-mamboleo.