Urusi imeishambulia tena Ukraine Jumamosi usiku, Februari 26, 2022, ikishusha makombora mawili katikati ya jiji la Kyiv kwa mujibu wa Reuters.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa kimeshuhudia kombora moja zito likishuka katika eneo lililo karibu na Uwanja wa Ndege wa Zhulyany, ikielezwa kuwa limepiga kituo cha mafuta.
Shuhuda mwingine ameeleza kuwa kombora jingine limeshuka katika eneo lililo karibu na jengo la Sevastopol Square, ambalo ni moja kati ya majengo marefu zaidi nchini humo.
Aidha, Serikali ya Ukraine imekiri kutokea kwa mashambulizi hayo, lakini imeeleza kuwa kombora moja limepiga jengo wanaloishi raia.
Hii ni siku ya nne tangu Urusi iingie rasmi kwenye jiji la Kyiv ikiwa na wanajeshi wanaoenda kwa mguu pamoja na kushusha makombora kadhaa. Makombora yake yamelenga maeneo muhimu katika siku hizo, ambapo moja lilitajwa kushuka katika kituo kikubwa cha mafuta.
Shinikizo laongezeka kwa Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema kuwa yeye ndiye mlengwa namba moja na familia yake namba mbili dhidi ya vikosi vya Urusi. Rais huyo ameahidi kubakia katika jiji hilo akikabiliana na Urusi.
Roman Abramovic ajiuzulu Chelsea FC
Juzi, Ukraine ilitangaza kuwa imewaua askari 2,800 wa Urusi na kwamba wanaendelea kuitetea ardhi ya nchi hiyo.
Kwa upande wa Urusi, Rais Vladimir Putin ameendelea kutoa wito kwa wanajeshi wa Ukraine kuweka silaha chini vinginevyo wataendelea kushambuliwa.