Baada ya bifu la Nicki Minaj na Cardi B kupoa kwa muda sasa  Nicki amehamishia majeshi kwa Miley Cyrus kwa kosa la kumchana Minaj kupitia wimbo wake wa hivi karibuni, Cattitude.

Rapa Nicki minaj ameamua kufunguka na kumtolea uvivu Miley Cyrus kupitia ‘episodi’ mpya ya kipindi chake cha Queen Radio ambapo Nicki ametoa siri za Miley  kutembea na watayarishaji wa muziki ili  wamtoe kimuziki na ameweka wazi mahusiano ya mtayarishaji wa muziki Mike Will na Miley Cyrus.

Aidha Nicki Minaj amesema kuwa imekuwa ni tabia ya Miley kutembea na baadhi ya watayarishaji wa muziki ili abaki kwenye chati na kujulikana zaidi.

Miley Cyrus alimchana rapa Nicki kwenye wimbo wa Cattitude ambapo aliimba “Ilove Nicki but I listen to cardi” yaani nampenda Nicki lakini namsikiliza Cardi.

Hatahivyo bifu la wawili hawa lilianza mwaka 2015 ambapo Miley alimkosoa Nicki Minaj kupitia New York  Times baada ya kulalamika kunyimwa tuzo ya video bora ya mwaka Anconda  kwenye MTV Awards.

Waziri ahojiwa kwa tuhuma za kupanga kumuua Makamu wa Rais
Askari 6 mbaroni kwa kuomba rushwa ya milioni 8 kwa mzee wa miaka 95