Shirika la Amnesty International, limesema kuwa kampeni ya kivita ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana na wanamgambo wa kundi la IS kutoka mji wa Raqqa nchini Syria, imesababisha vifo vya raia wengi nchini humo.
Shirika hilo la Kutetea Haki za Binaadamu – Amnesty International limesema kuwa vikosi vya serikali ya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vimefanya mashambulizi ya kutochagua maeneo hali iliyopelekea raia wengi kuendelea kuangamia kusini mwa mji wa Raqqa.
Aidha, Jeshi la Kidemokrasia la Syria (SDF) la muungano wa wapiganaji wa Kiarabu wa Kikurdi liliingia katika mji huo mwezi Juni, na hadi kufikia sasa jeshi hilo limeweza kuushikilia mji huo kwa asilimia 60 kutoka kwa wanamgambo wa IS.
“Kwa vile vikosi vya SDF na vya Marekani vinajua kwamba kundi la IS linawatumia raia wa mji wa Raqqa kama ngao ya kivita, inatakiwa iongezwe nguvu na jitihada za kuwalinda raia hasa kwa kupunguza mashambulizi pamoja na kutengeneza njia salama,” amesema Donatella Ronvera Mshauri Mkuu wa Masuala ya Migogoro wa Amnesty International.
-
Marekani, Korea Kusini zaungana kufanya mazoezi ya kijeshi
-
India yafuta sheria ya kuwapa talaka wanawake kirahisi kwa ‘WhatsApp’
-
Rais Maduro akabiliwa na tuhuma za rushwa
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa umesema kuwa inakadiria kwamba kuna raia 25,000 bado wamebaki ndani ya mji huo, lakini wengine wameukimbia ili kuweza kujiokoa na kuokoa mali zao kufuatiwa IS kuweka kambi katika mji huo.