Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, linakadiria kwamba malori 100 yaliyobeba misaada yalihitajika kufika Tigray, Ethiopia kila wiki ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya watu milioni tano, lakini kulingana na ugumu wa kufika eneo hilo ni 12% ya misaada iliyohitajika iliyoweza kufika katika jimbo hilo.
Surafeal Mearig mwenye umri wa miezi mitatu amelala bila msaada wowote katika hospitali kubwa zaidi katika jimbo lililokumbwa na vita la Tigray.
Macho yake yamefunguka wazi, na mbavu zake zinaonekana zikipanda na kushuka zikiwa nyembamba zenye makunyanzi. Ni miongoni mwa watoto wengi wanaoumia kutokana na utapiamlo, kwasababu ya vita vya wenywe kwa wenyewe vya miezi 14 ambavyo vimesambaa katika majimbo jirani ya Afar na Amhara.
Daktari wa watoto anayemshugulikia Surafeal katika hospitali ya rufaa ya Ayder Referral katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ana uzito wa mwili wa kilo 2.3, kilo moja chini ya kilo alizokuwa nazo alipozaliwa.
Kulingana na maelezo kwa waandishi wa habari yaliyochapishwa na mhudumu wa hospitali, maziwa ya mama yake yalikuwa yamenyauka na wazazi wake, ambao wote hawana ajira, hawawezi kununua maziwa ya watoto ili kuweza kumpatia mtoto wao.
Muhimu ni kwamba mhudumu wa hospitali anasema wanaishiwa na vyakula vinavyoweza kuwatibu watoto utapiamlo kama Surafeal.
“Ni miezi sita sasa tangu tusambaziwe vyakula hivi kutoka Adis Ababa ( mji mkuu wa serikali kuu ya shirikisho],” daktari ambaye hakupenda jina lake katika hospitali aliliamba shirika la habari la BBC kwani anahofia familia yake kufuatiliwa.
“Tunakaribia kumaliza kile tulichokuwa tumepewa tangu msaada wa kwanza ulipowasili mwezi Juni. Kila kitu kinaisha,” aliongeza.
Wiki hii wafanyakazi wa tiba katika hospitali ya Ayder waliwasilisha ripoti kwa mashirika ya kimataifa ya misaada wakiomba usaidizi.
Surafeal alikuwa mmoja wa wale waliotolewa kama mfano wa watoto wenye ukosefu wa msaada wa lishe.
Madaktari wanasema zaidi ya 40% ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wanaokuja hospitali wanakabiliwa na utapiamlo- mara dufu ya kiwango cha mwaka 2019.
Medhaniye ambaye alizaliwa akiwa mwembamba pia amelala kwenye kitanda cha hospitali , akila kwa kutumia mrija uliounganishwa kupitia puani kwake.
Ripoti yake ya matibabu inasema alianza kuugua kutokana na utapiamlo baada ya wanajeshi kuishambulia nyumba ya familia yake na kuwachinja ngobe, kuharibu na kupora mali zao.
Kulingana na shirika la habari la BBC halikuweza kupata duru huru za kuthibitisha maelezo hayo katika ripoti ya daktarin kwani kwa kiasi kikubwa Tigrai imekuwa haina mawasiliano tangu mwezi Novemba 2020, wakato mzozo ulipoibuka baina ya wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF), ambao wanadhibiti eneo kubwa la jimbo, na serikali ya shirikisho.
Waandishi wa habari hawajaweza kutembelea Tigray tangu mwezi Julai. July.
Lakini tangu vita vilipoanza, mashirika ya misaada yamekuwa yakilalamika kuhusu kutoweza kupata taarifa za kutosha ndani ya Tigray.
Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya haki za binadamu (Ocha) tarehe 30 Disemba, msafara wa magari ya msaada haujafika bado Tigray tangu katikati ya mwezi wa Disemba kwasababu ya urasimu wa ucheleweshaji na ukosefu wa usalama.