Vituo viwili vilivyoonyesha picha za maandamano yaliyopangwa kupinga kukamatwa kwa Ousmane Sonko, ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha PASTEF, kwa madai ya “kuvuruga utaratibu wa jamii” vilikatizwa, na kupunguzwa matumizi yao kwenye mitandao ya kijamii.

Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika kote nchini kumuunga mkono Sonko, ambaye kinga yake ya Bunge iliondolewa mnamo Februari 26 kwa sababu ya mashtaka ya ubakaji na kuzuiliwa wakati akienda kutoa ushahidi mnamo Machi 3 kuhusu kesi hiyo.

Matumizi ya mitandao ya kijamii yalizuiliwa kabla ya maandamano, na viunganishi vya mtandao wa internet vilikatizwa kikamilifu kwenye laini kadhaa za rununu.

Vituo vya Wolf TV na Sen TV vilivyotangaza maandamano ya barabarani ambayo yalizuka siku Sonko alipowekwa kizuizini pia vilikatizwa kwa masaa 72 kufuatia uamuzi wa Baraza la Udhibiti wa Utangazaji (CNRA).

Kiongozi huyo wa upinzani, ambaye bado yuko chini ya ulinzi na anatumia haki yake ya kukaa kimya wakati wa kuhojiwa, anatarajiwa kupelekwa mahakamani na kutoa ushahidi ndani ya siku.

Wanafunzi 1,194 wakatisha masomo kwa ujauzito
Papa Francis awataka Iraq kuepuka vurugu, mivutano ya kidini