Tamko la Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu uwekezaji katika Rasilimali Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam Julai 2023, litakuwa sehemu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 43 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC, unaondelea jijini Luanda, Angola.

Kauli hiyo ilitolewa Agosti 13, 2023 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax wakati anaongea na Vyombo vya Habari pembezoni mwa mkutano huo akisema tamko la Dar es Salaam limeainisha masuala mbalimbali ya utekelezaji kwa ajili ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Antipas Nyamwisi (kulia) akikabidhi uenyekiti wa baraza hilo kwa Waziri wa Uhusiano wa Nje wa Angola, Téte António.

Masuala hayo, yameendelea kujadiliwa katika Mkutano wa 43 wa SADC ili kuhakikisha kuwa, katika kutekeleza kaulimbiu ya mwaka huu ambayo inahusu umuhimu wa rasilimali watu na fedha katika maendeleo endelevu ya viwanda, tamko la Dar es Salaam linakuwa sehemu ya utekelezaji wa kaulimbiu hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, akifuatilia hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Luanda, Angola tarehe 17 Agosti 2023.

“Suala la uwekezaji katika rasilimali watu, suala la uendelezaji wa rasilimali watu katika kuendeleza uchumi, ni vitu ambavyo tunaendelea kuvisukuma kama ilivyokuwa kwa Rais wetu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo uliofanyika Tanzania,” alisema Dkt. Tax.

TAKUKURU yapewa agizo ubadhirifu fedha za Serikali
Viongozi wa Dini wawaingilia kati mzozo ECOWAS, Jeshi la Niger