Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imethibitisha mpango wa kuviboresha viwanja vya michezo nchini kwa kuviwekea Nyasi Bandia.
Uthibitisho huo umetolewa leo Jumanne (Juni 14) na Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nhemba, alipokua akisoma makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti ya 2022/23) ya Serikali, Bungeni mjini Dodoma.
Waziri Nchemba amesema kwa kuanzia, Serikali itaanza kuviwekea Nyasi Bandia viwanja vitano, na kisha vingine vitafuata.
“Kwa kuanzia tutaweka Nyasi Bandia katika viwanja vya mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha, Tanga na Mbeya” amesema Waziri Mwigulu Nhemba.
Kuboreshwa kwa viwanja vya CCM Kirumba, Sheikh Ameri Abeid, Mkwakwani, Sokoine na Jamhuri kutanogesha ushindani zaidi katika Mshike Mshike wa Michezo ya Ligi Kuu na madaraja ya chini kwa msimu ujao wa 2022/23.