Mlima Nyiragongo, uliopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeshuhudiwa ukitoa mawingu makubwa ya moshi mweusi na kurusha majivu ya volkano angani.
Mlima huo ambao umebeba mojawapo ya volcano zinazoendelea kutokota duniani, umeshuhudiwa kuanzia Januari mosi, 2022 ukivujisha lava na kadri siku zinavyosogea ndivyo lava inaongezeka.
Wanajiolojia kutoka Kituo cha Kuchunguza Volcano cha Goma wanasema bado hakijatiririka, lakini wameona ongezeko la mitetemmaeneo ya jirani na mlima huo.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Celestin Kasereka, aliambia shirika la habari la BBC kwamba milipuko ya hapa na pale ndiyo iliyosababisha moshi na majivu ambayo yanaweza kuonekana katika jiji lote la Goma lakini akisisitiza kuwa pamoja na hayo, Nyiragongo huenda isilipuke tena.
Wakazi wa maeneo hayo wameshauriwa kuwa watulivu, lakini hili litakuwa gumu kwa wengi, kwani athari mbaya iliyosababishwa na mlipuko wa Mei 2021 bado ni mbichi akilini mwao.