Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imetangaza ratiba ya msimu mpya wa Ligi kuu 2020/21, ambao umepangwa kuanza rasmi Septemba 06.

Katika ratiba hiyo iliyotangazwa muda mchache uliopita, Mabingwa watetezi Simba SC wataanza kutetea taji lao mbele ya Ihefu FC ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu, wakitokea Ligi Daraja la Kwanza.

Katika mchezo huo SImba watakua ugenini kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Wakati Simnba wakianzia ugenini watani zao wa jadi Young Africans watabaki jijini Dar es salaam kupapatuana na maafande wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons FC

Ratiba kamili ya michezo ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lebanon: Rais Aoun akata kujiuzulu
Rasmi Rais Magufuli kukabidhi uenyekiti wa SADC

Comments

comments