Matamshi yaliyotolewa na kiungo Kevin De Bryne, 24 kuwa atabakia Wolfsburg msimu ujao yamepuuzwa na wakala wake na hivyo kuwepo bado na uwezekano wa uhamisho wa pauni milioni 50 kwenda Manchester City (Times)

Chelsea wametoa dau jingine jipya la pauni milioni 30 kumtaka beki John Stones, 21, lakini huenda fedha hizo zikaongezeka kwa pauni milioni 10 zaidi ili kufanikisha uhamisho huo kutoka Everton (Telegraph)

Meneja wa Chelsea pia atapewa fedha zaidi na Roman Abramovich kununua wachezaji wengine wawili kabla dirisha la uhamisho halijafungwa kufuatia kuanza vibaya msimu mpya (Daily Mirror)

Everton watamwania, ama- Ashely Williams, 30, wa Swansea au Kalidou Koulibaly, 24 wa Napoli, iwapo Stones ataondoka Goodison Park (Daily Star)

Arsenal na Manchester United wametaarifiwa uwepo wa Zlatan Ibrahimovic, 33, ambaye ameambiwa na klabu yake ya PSG kuwa anaweza kuondoka kwa bei nafuu (Daily Mail)

Manchester City wameambiwa waongeze dau kama wanamtaka beki wa Valencia Nicolas Otamendi (Sky Sports)

City hawatomruhusu Eliaquim Mangala, 24, kwenda Valencia kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Otamendi (Daily Express)

Mkurugenzi mkuu wa Manchester United Ed Woodward amekwenda Barcelona kujaribu kukamilisha uhamisho wa Perdo (Daily Mail)

Newcastle wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin kutokana na bei yake ya pauni milioni 15 (Newcastle Chronicle)

West Ham bado wanataka kumsajili Austin (Evening Standard)

Newcastle wanakaribia kumsajili winga wa Marseille Florian Thauvin, 22, katika mkataba ambao Remy Cabella, 25, atakwenda Ufaransa (Guardian)

Juventus huenda wakamsajili Eric Lamela, 23, kutoka Tottenham iwapo watashindwa kumsajili Christian Eriksen, 23 (Evening Standard)

Sunderland wanataka kumrejesha tena mchezaji kiraka wa Aston Villa Kieran Richardson, 30 (Daily Mirror)

Southampton wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 24 kwa pauni milioni 8.5 na bado pia wanamtaka beki wa kati wa Celtic Virgil van Dijk (Daily Star)

Sunderland wana wasiwasi watashindwa kumsajili Fabio Borini wa Liverpool na watazidiwa kete na Inter Milan (Sunderland Echo)

West Brom wamepanda dau la pauni milioni 5 kumtaka Federico Fazio wa Tottenham (Telegraph)

Norwich wanataka kumsajili Mattia Destro kwa mkopo kutoka Roma (Times)

Kipa wa Manchester United atatafakari kumfukuza kazi wakala wake Jorge Mendes iwapo hatofanikisha uhamisho wake kwenda Real Madrid kabla ya dirisha la usajili kufungwa (Independent).

Ali Kiba Na Neyo, Kazi Imeanza
Stars Kumkosa Mshambuliaji Wa Mansfield Town