Bodi ya Ligi (TPLB) imeufungia uwanja wa Majimaji kutopokea Mashabiki katika mechi zilizosalia msimu huu, hadi hapo ulinzi na usalama utakapoboreshwa.
Uwanja huo umefungiwa kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mchezo uliopita wa Ligi daraja la Kwanza kati ya wenyeji Mlale FC dhidi ya Dodoma FC.
Klabu ya Mlale FC ya Ligi daraja la Kwanza imepigwa faini ya laki tano na bodi ya Ligi kwa kitendo cha kuanzisha vurugu kwa kumpiga refa katika mchezo wao uliopita dhidi ya Dodoma FC zilizosababisha mchezo huo kuvunjika
Aidha Dodoma FC imepewa ushindi wa mabao matatu pamoja na alama tatu kwenye mchezo huo.
Nae kocha msaidizi wa klabu ya Mlale FC Rashid Mpenda amefungiwa miezi sita na faini ya Tsh. 300,000 kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati na mwamuzi msaidizi namba mbili katika mchezo uliopita wa Ligi daraja la Kwanza dhidi ya Dodoma Fc uliopigwa katika uwanja wa Maji Maji Songea