Munge wa Viti maalumu, Ester Bulaya amesema hapendezwi kuona malumbano baina ya Vyama vya Siasa nchini hasa vya upinzani na badala yake kuvitaka kuwa na ushirikiano kwa lengo la kukitoa Chama Cha Mapinduzi madarakani.
Bulaya ameyasema hayo hivi karibuni jijini Dodoma wakati akifanyiwa mahojiano maalum na Dar24 Media na kuelezea umuhimu wa vyama vya upinzani kuungani na kuwa kitu kimoja ili kuleta chachu katika maendeleo ya Taifa na kujenga utawala bora.
Amesema, ‘’mimi sipendi malumbano ya vyama vya upinzani, mimi naamini tutaitoa CCM madarakani na mbaya zaidi mfumo wa Chama cha Mapinduzi umejiweka ni chama dola kwahiyo tunahitaji ushirikiano bila kuwa na wivu tusione kwamba tukishirikiana na CHADEMA tutaipa nguvu au tukishirikiana na NDC nitaipa nguvu hapana.”
Aidha Bulaya ameongeza kuwa, “CCM na Dola yake wanagawa watu ili wawatawale, mimi naamini kwenye solidarity na haimaanishi mkiungana kuna vyama vitamezwa no mnaunganisha nguvu moja muweze kupambana na yule adui yenu muweze kushinda vita.’’
Hata hivyo, Bulaya amempongeza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa umuzi wa maridhiano ambao umeleta matokea chanya kwa vyama vyote vya siasa nchini na kwamba kutoka kwake Gerezani na kwenda Ikulu haina tofauti na Nelson Mandela aliyetoka Gerezani kwenda kukaa na makaburu ili kuifanya Afrika ya Kusini kuonekana hivi ilivyo leo.