Vyombo vya Habari nchini, vimetakiwa kuanzisha Dawati la kijinsia kwa lengo la kukabiliana na rushwa ya ngono na mfumo dume katika vyumba vya habari.
Wito huo umetolewa na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari kwenye mkutano was uliofanyika Desemba 16, 2022, jijini Dar es Salaam.
Mwendasha mada na Waikili, James Marenga amesema wanawake wanapaswa kupewa nafasi walau asilimia 30 kwenye vyombo vya habari, na kuhoji sababu za jinsia hiyo kuwa chache kwenye tasnia.
Hata hivyo, wasiriki walichangia kuwa miongoni mwa sababu kwa wanawake kupata nafasi za chini katika vyombo vya habari, ni kutojiamini, mfumo dume na rushwa ya ngono.
Mhariri Gazeti la Mwananchi, Lilian Timbuka alisema “Kuna tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyumba vya habari, nah ii husababishwa na baadhi ya wanawake kwenye vyumba hivyo vya habari kutojiamini lakini pia mfumo dume,”
Imeelezwa kwamba, kuanzishwa kwa madawati ya jinsia katika vyumba vya habari kutatoa fursa kwa wale watakaofanyiwa matukio kinyume na maadili ya tasnia hiyo, kuwa na mahali pa kupata msaada.
Akichangia mada hiyo, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alisema alisema Mona ya sababa za wanawake kuangukia kwenye rushwa ya ngono katika vyumba vya habari zinatokana na ugeni.
Alisema, “Nashauri kuwe na utaratibu kwamba wakiwa mwaka wa pili, waweze kuingizwa katika vyombo vya habari mara kwa mara walau wapate uzoefu kabla ya kumaliza masomo yao.”
Kuhusu asilimia 30 wanawake kwenye vyumba vya habari, Balile alisema kuwepo kwa sheria hiyo ambayo imependekezwa katika vikao vya maoni ya wadau wa habari na serikali, kutasaidia kumlazimisha mwajiri kuajiri wanawake.