Vyombo vya habari nchini hasa vile vya kijamii vimeshauriwa kuwaepuka wanasiasa katika uendeshaji wa kazi zao ili vizingatie dhumuni kuu la kuelimisha wanajamii katika kuleta maendeleo ya Jamii.
Hayo yamesemwa na leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo yahusuyo Radio ya Jamii kwa Maendeleo Vijijini kwa waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Amesema kuwa Redio za Jamii zinatakiwa kusimamia malengo yao makuu ya kuwa karibu na jamii husika na kuzifanya jamii hizo kunufaika na Redio hizo na sio kufarakanisha jamii.
“ Nisistizie kwa washiriki kuzingatia malengo ya mafunzo haya mnayopewa ili yasaidie katika kuielimisha jamii katika masuala mbalimb ali na kuachana na masuala ya siasa,” amesema Anastazia.