Rais Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia ulinzi na Sheria za barabarani kuongeza juhudi za udhibiti ajali hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka na amewataka madereva kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Rais Samia ameyasema hayo kati taarifa yake aliyoitoa ya salamu za rambirambi kwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kufuatia vifo vya watu 14 waliofariki katika ajali ya barabarani kijiji cha Lidumbe, wilaya ya Newala.

Kwa Mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mtwara, ACP, Mark Njera vifo hivyo vilitokea tarehe 2 Januari saa 2.15 usiku katika barabara ya Mtwara-Masasi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa Lori aina ya Scania ambapo alishindwa kulimudu na kuwagonga watu hao na wengine 22 waljijeruhiwa.

Taarifa yenye salamu za rambirambi kutoka Ikulu

Uamuzi mdogo wa pingamizi kesi ya Sabaya kutolewa leo
Pasta awaogesha wanawake wakiwa watupu kuwapa 'upako wa ndoa'