Vyuo 22 vimeitunishia misuli Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), juu ya agizo la kuwasilisha orodha ya majina ya wanafunzi waliosajiliwa kwaajili ya kuhakiki sifa zao.

Tume hiyo iliviagiza vyuo vikuu vyote nchini kuwasilisha majina ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza 2015/2016, ili kuhakiki sifa zao.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa TCU, Edward Mkaku, amesema kuwa januari 9, mwaka huu ndio ilikuwa siku ya mwisho kupokea taarifa ya vyuo hivyo.

Aidha, Mkaku amesema vyuo ambavyo vimekiuka agizo hilo vitachukuliwa hatua ya kisheria kwa mujibu wa kanuni za usajili ya 62(2) (a)(b) ya mwaka 2013, amesema kanuni hiyo itakwenda sambamba na kufutiwa usajili wa wanafunzi hao ambao wanaosoma shahada ya kwanza kwenye vyuo hivyo.

Mkaku amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Community Development Training Institute (CDTI), Arusha Technical College, Ms Training Center for Development Cooperation na College of Business Education Dar es salaam (CBE).

Vingine ni Institute of Adult Education, Institute of Procurement and Supply, Center for Foreign Relations Dar es salaam, Unique Academy Dar es salaam, Zanzibar Institute of Financial Administration, The Mwalimu Nyerere Memorial Academy Zanzibar.

Hata hivyo Mkaku amesema vingine ni Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology, University of Arusha, St.Augustine University of Tanzania (Arusha Center), Josiah Kibira university College, The Open University of Tanzania (OUT), University of Dodoma, University of  Iringa, Zanzibar University, Tumaini University (Mwanza) na University of Arusha (Buhare Center) amesema Mkaku.

 

 

JPM awasili Simiyu, aweka jiwe la msingi Hospitali ya mkoa
#HapoKale