Mashabiki wanane, wameripotiwa kutiwa nguvuni na jeshi la polisi jijini London, wakati wamchezo wa ligi ya nchini England, uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kati ya Arsenal dhidi ya Tottenham Hospurs.

Jeshi la polisi jijini London, limethibitisha kuwatia nguvuni watu hao, kutokanana uharibifu uliofanywa kwenye vyoo vya uwanja wa Emirates, wakati mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Spurs ukiendelea kwenye uwanja wa Emirates.

Pamoja na kutolewa kwa taarifa hizo, bado haijafahamika ni mashabiki wa klabu gani kati ya hizo mbili, wanaoshikiliwa na jeshi la polisi, japo vyoo vilivyoharibiwa vilikua vya upande wa majukwaa yaliyotumiwa na mashabiki wa Spurs.

uharibifu

Taarifa za awali baada ya uharibufu huo kubainika kufanyika kwenye vyoo vya uwanja wa Emirates usiku wa kuamkia jana, zilieleza kwamba, huenda mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Spurs walifikia hatua ya kufanya hivyo, kama ishara ya kulipiza kisasi kutokana na uharibifu wa mabango ya majukwaani ambao ulifanywa na mashabiki wa Arsenal kwenye uwanja wa White Hart Lane mwezi septemba wakati wa mchezo wa kombe la ligi, (Capital One Cup).

Mpaka uthibitishwa wa kukamatwa kwa mashabiki hao wanane unatolewa na jeshi la polisi, bado viongozi wa Arsenal hawajasema lolote juu ya thamani ya kamili ya vyoo vilivyoharibiwa kwa kuvunjwa vunjwa.

Katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, Arsenal walifanikiwa kujinusuru kupoteza nyumbani, kufuatia bao lililofungwa na beki wa pembeni Kieran Gibbs baada ya Spurs kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Harry Kane.

Steve McClaren Kuingia Vitani Na Slaven Bilic
Muhimbili Yalaani Kilichofanywa na Waandishi Wa Habari, Rais Magufuli Alipofanya Ziara ya Kushtukiza