Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetengaza orodha ya waamuzi 17 waliopata beji za Shirikisho la Soka duniani (FIFA) kwa mwaka 2021.

TFF wametangaza orodha hiyo, baada ya kuipokea kutoka FIFA ambao wanaratibu zoezi wa kutoa beji hizo kwa waamuzi waliofikia viwango vinavyotambuliwa kimataifa.

Mwamuzi Hery Sasii ambaye usiku wa kuamkia jana alizua songombingo baada ya kutoa mkwaju wa Penati tata kwenye mchezo wa Simba SC dhidi ya KMC FC, ni miongoni mwa waamuzi waliotajwa kwenye orodha hiyo.

Sasii alitoa mkwaju wa Penati kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam na kuiwezesha Simba SC kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri, kupitia kwa mshambuliaji Meddie Kagere.

TAARIFA yenye orodha ya waamuzi waliopata beji ya FIFA iliyotolewa na TFF;

Rais wa zamani wa Burundi afariki dunia
Busquets aingia anga za Messi FC Barcelona

Comments

comments