Kamati ya Marefa ya shirikisho la soka barani ulaya Uefa imeteua waamuzi 18 kwa ajili ya michuano ya ulaya itakayofanyika huko nchi Ufaransa mwaka 2016.

Waamuzi hao watachezesha michezo 51 ya michuano hiyo ya ulaya itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 10 na kumalizika Julai 10 mwaka 2016.

Katika kila mchezo mmoja watatumika waamuzi watano kama iliyokua katika michuano ya Euro ya mwaka 2012, kutakua na mwamuzi wa kati akisaidiwa na waamuzi wawili wa pembeni na wengine wawili katika kila goli.

Orodha ya mwisho ya waamuzi watakaochezesha fainali hizo itatolewa mwezi Februari mwakani na kamati hiyo ya waamuzi.

Mrithi Wa Andrey Coutinho Asaini Mwaka Mmoja Yanga
MSN Ya FC Barcelona Si Lolote Kwa UEFA