Kumezuka maandamano dhidi ya serikali katika miji yote ya Iran, kufuatia kujibu kifo cha Msichana mmoja Mahsa Amini (22), aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi wa maadili ya nchi, ambapo vyombo vya habari vimesema vikosi vya usalama vilifyatua risasi zilizoelekezwa katika umati wa watu na kuwaua wanaume wanne.

Maandamano hayo, yalizuka katika miji kumi yenye kampasi za vyuo vikuu mjini Tehran ambayo yalichochewa na kifo hicho kilichotokea Septemba 17, 2022 cha binti huyo, ambaye aliyekamatwa mjini Tehran kwa madai ya kukiuka sheria ya Iran ya hijab, ambayo inawataka wanawake kufunika nywele zao na kuvaa majoho.

Mahsa Amini (22), anayedaiwa kufariki akiwa chini ya ulinzi wa Polisi na kuamsha ghasia kwa Taifa la Iran. Picha na alliance.

Wanawake waliokuwa wakiandamana siku ya Jumatatu (Septemba 19, 2022), walivua vitambaa vyao vya kichwa na kuvipungia mkono kwa dharau Huko Tehran, ambapo wanaume na wanawake waliimba, “tutapigana na kurudisha nchi yetu,” wakiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu, hali ambayo inaweza kusababisha marufuku ya maisha ya elimu ya juu.

Vikosi vya usalama, katika mji mkuu wa nchi hiyo Tehrain, vilifyatua risasi na maji ya kuwasha, kuwakimbiza waandamanaji na kuwapiga kwa marungu, tukio ambalo limesambaa katika mitandao ya kijamii kupitia video zilizorushwa na waandishi wa Habari, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakionya hatua hiyo.

Mabadiliko Ligi Kuu yazibeba Simba SC, Young Africans
Waziri Mkuu kuwasilisha mipango mapambano ya uchumi