Polisi mjini Hong Kong imesema kuwa takriban watu 90 wamekamatwa jana wakati wa maandamano dhidi ya uamuzi wa serikali kuahirisha uchaguzi wa bunge wa eneo hilo.

Wakosoaji wa Lam, wanasema serikali yake ina hofu kwamba upande wa upinzani utajinyakulia viti zaidi iwapo uchaguzi huo ungefanyika kama ulivyopangwa.

Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike jana lakini Julai 31, kiongozi mkuu wa Hong Kong, Carrie Lam aliuahirisha kwa mwaka mmoja kutokana na ongezeko la virusi vya corona.

Maandamano dhidi ya serikali yamefanyika mjini Hong Kong karibu kila siku za mwisho wa juma, tangu Juni 2019, maandamano yaliyochochewa na pendekezo la kuhamishwa kwa washtakiwa kutoka eneo hilo hadi China bara.

Wanaojitokeza tokeza wataisoma namba - Magufuli
Kagera kuongoza uzalishaji wa kahawa