Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya waandamanaji wanaopinga utawala wa Rais, Joseph Kabila umesababisha vifo vya watu takribani 47.

Imesema kuwa kati ya tarehe 1 Januari mwaka jana na tarehe 31 Januari mwaka huu, watu wasiopungua 47 waliuawa na maafisa wa polisi wakati wa maandamano na kuongeza kuwa kulikuwa na jaribio la vyombo vya dola kufunika ukweli.

Aidha, Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa na Mjumbe wa Umoja huo kwa Congo, Zeid Ra’ad Al Hussein, pamoja na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Congo, Leila Zerrugui, wamesema kuwa ripoti hiyo imeonyesha mauaji na matukio mengine mabaya ya ukiukwaji wa haki za binaadamu, yametokana na utumiaji wa nguvu kupita kiasi.

Hata hivyo, Maandamano yalianza kushika kasi nchini humo miezi kadhaa iliyopita mara baada ya Rais Kabila kukaidi kuondoka madarakani baada ya muda wake kufikia mwisho Desemba 2016.

 

Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond
Rais Mstaafu ashikiliwa na Polisi