Vikosi vya usalama nchini Sudan vimerusha mabomu ya machozi kwa waandamanaji ambao wanapigania demokrasia katika mji mkuu wa Khartoum.

Walimu waliokuwa wakishiriki katika mojawapo ya maandamano hayo walikamatwa na vikosi vya usalama ikiwa usiku kucha, waandamanaji waliweka vizuizi kwa siku mbili za kwanza za maandamano ili kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Wanataka serikali ya kijeshi kujiuzulu na kuruhusu mabadiliko ya amani.

Maandamano hayo yanafanyika huku wapatanishi wa Muungano wa mataifa ya Kiarabu {Arab League} wakiwasili mjini Khartoum kwa mazungumzo ili kujaribu kusitisha tatizo hilo.

Waziri mkuu Abdalla Hamdok, bado amewekwa katika kifungo cha nyumbani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa wanajeshi hao kushirikiana nao.

Mwezi uliopita , kiongozi wa mapinduzi hayo Jenerali Abdel Fattah al – Burhan , alifutilia mbali utawala unaoongozwa na raia, kuwakamata viongozi wa kiraia na kutangaza hali hatari.

Kansela Angela Merkel anena na vijana
Sababu za wapinzani wa Simba SC kuambulia kadi nyekundu zaanikwa