Waandamanaji na wafuasi wa kiongozi wa kidini wa Iraq Moqtada al-Sadr wamevamia bunge kwa mara ya pili wiki hii ambapo walionekana wakiimba na kucheza baada ya kuwazidi nguvu maafisa wa usalama.
Hata hivyo vikosi vya usalama vya Iraq vilipambana na maelfu ya waandamanaji katika mji wa Baghdad kwenye eneo linalojulikana kama Green zone.
Waandamanaji walitumia Kamba kuvuta vizuizi vilivyoundwa kwa simenti ili waweze kufikia lango kuu la Green zone ambako majengo ya ofisi na balozi za kigeni vipo.
Polisi wa Iraq walitumia gesi ya machozi na mabomu yenye sauti kubwa kutawanya waandamanaji wakati walipokuwa wanasogea katika jengo la bunge.
Al- Sard aliitisha maandamano kupinga kuunda serikali mpya inayoungwa mkono na makundi ya kisiasa ya Iran wakati kipindi cha bunge la kawaida kikitarajiwa kuanza.
Chama cha Al-Sadr kiliondoka katika mazungumzo ya kuunda serikali mwezi Juni na kuruhusu wapinzani wake katika kamati ya uratibu kufikia wingi unaohitajika kuendelea na utaratibu.