Afarah Suleiman – Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amewataka Waandishi wa Habari wa Mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro kuhabarisha umma juu ya elimu waliyoipata juu ya matokeo ya sensa ya watu na makazi, iliyofanyika mwaka 2022.
Mongela ambae alikuwa mgeni rasmi katika Semina ya Waandishi wa habari inayohusu Usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, ametoa wito huo hii leo Ocktoba 24, 2023 jijini Arusha.
Amesema, pia Viongozi wa Ofisi ya Takwimu nao wanatakiwa kuendelea kutoa elimu kila mahali juu ya matokea ya sensa, ambapo kwa mkoa wa Arusha kuna ongezeko la asilimia 3.2 kutoka watu zaidi ya milioni moja na laki sita hadi kufikia zaidi ya watu milioni mbili na laki tatu kwasasa.
Awali, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makaz, Anne Makinda amesema kundi la Wanahabari ni muhumu katika jamii kwani linawanawafikia watu wengi, hivyo amewataka kufanya kazi bila hofu na kufikisha elimu ambayo wameipata kwa Wananchi.
Kwa upande wao baadhi ya Wanahabari walioshiriki mafunzo hayo, wamesema yamewasaidia kuwa na upeo wa kufahamu zaidi juu ya Takwimu za kiuchumi, kijamii na mazingira Kwa ujumla na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha wanaielimisha jamii kwa kuchambua kipengele kimoja kimoja kwa ufasaha.