Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein All Mwinyi ametoa wito kwa tasnia ya habari kuitumia fursa ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kuweka mkazo kwenye uhuru wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za Binadamu, kwa kuangazia uhusiano baina ya uhuru wa vyombo vya habari na haki nyengine.

Rais Dkt. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani katika ukumbi wa hotell ya Golden Tulip uliopo Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi hii leo Mei 3, 2023.

Amesema, waandishi wa Habari wanatakiwa kutimiza ahadi zilizotolewa na kila nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa i kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu na wadau wa vyombo vya habari kuisherehekea siku hiyo kwa kuungana na mashirika yanayotangaza masuala ya mazingira, haki zo
wanawake, watoto, haki za kiasili, haki za kidijitali, vita dhidi ya ufisadi.

Kuhusu sheria ya Habari, Dkt. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar layari imeandaa muswada wa sheria hiyo yenye madhumuni ya kufuta Sheria iliyopo ya Usajili wa Magazel, Wakala wa Habari na villabu Sheria nambari 5 ya mwaka 1988 ambapo marekebisho yake ni sheria nambari 8 ya mwaka 1997 na kutunga Sheria mpya ya Huduma za Habari na Mambo yanayohusiana na hayo.

Aidha, alieleza kwa Zanzibar, magazeti na majarida 71 yamesajiliwa tangu mwaka 1998. Shirika la Utangazaj Zanzibar (ZBC) na Shirika la Magazeti ya Serikali ni vyombo vya habari vya Serikali ambavyo navyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa za kutoa taarifa kwa umma.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi mwezi Februari mwaka huu, jumla ya redio 218, televisheni 68. redio za mtandao nane, televisheni za mtandao 391, blog, majukwaa 73 na cable operators 53 zimesajiliwa Tanzania bara, ambapo baada tu ya uhuru wa Tanganyika kulikuwa na kituo kimoja tu cha redio cha Tanganyika.

Malipo ya Mvinyo badala ya pesa yalivyolibua simanzi
Tanzania mafunzoni ongezeko la thamani mazao ya chakula