Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali Mkoani Arusha wametimuliwa kwa kupigwa na mawe ambayo hayajulikani yanapotokea katika Kijiji cha Kiwawa Kata ya Imbasei Wilayani Arumeru.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni baada ya Waandishi hao kufika kwenye eneo hilo kwa lengo la kufuatilia taharuki ya Wananchi kupigwa kwa mawe yanayohisiwa kurushwa na Mizimu.
Katika tukio hilo Mwandishi wa GADI TV amejeruhiwa sehemu ya kichwani kwa kupigwa na jiwe huku mwandishi GLOBAL TV akijeruhiwa mkono wake wa kushoto.