Zaidi ya watu 50 kutoka nchini Ghana waliokuwa wakijaribu kuingia nchini Australia wakidai kuwa waandishi wa habari wanaoenda kuripoti habari za mashindano ya madola (Commonwealth games) walikamatwa baada ya kushindwa kujibu maswali rahisi kuhusu michezo.

Watu hao waliobainika kuwa walijidai kuwa waandishi ili wapate kuingia nchini humo kirahisi walishikiliwa na baadaye kufukuzwa licha ya kuwa na nyaraka zote sahihi za kusafiria.

Imeelezwa kuwa maafisa wa uhamiaji walibaini njama za watu kuingia nchini humo kwa mgongo wa mashindano hayo huku wakiwa na shughuli zao binafsi, hivyo waliandaa maswali ambayo ni ya kawaida kwa watu wanaofuatilia michezo.

Naibu Waziri wa Michezo wa Ghana, Pious Enam Hadidze, amesema kuwa wameanza kufanya uchunguzi kuhusu sakata hilo ili kubaini kama kuna udanganyifu uliofanyika katika kuwapa vibali.

Baadhi ya watu waliotimuliwa walikiambia kituo cha radio cha Atinka FM kuwa maafisa wanaohusika na kamati ya mashindano ya Olympics pamoja na Wizara ya Michezo walikuwa wanapokea kati ya $2,000 na $5,000 ili kusaidia kupata visa.

 

Zitto awataka Wazee wa Kigoma kuingilia kati suala la Nondo
Msajili atakiwa kufuta vyama vya siasa 'korofi'