Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans meweka mzigo wa maana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanatinga hatua ya makundi ya Ligi ya   Mabingwa Afrika, kwa kuitoa Al Merreikh ya Sudan.

Young Africans kesho Jumamosi (Septemba 30) wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Al Merrikh katika mchezo ambao kama watapata matokeo mazuri basi wataweka rekodi mpya ya kutinga hatua ya makundi ya ligi hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi kirefu.

Rais wa Young Africans, Injinia Hersi Saidi kuelekea katika mchezo huo amesema kuwa: “Sisi kama viongozi niwahakikishieni kuwa tunafanya kazi yetu na kwenye suala la motisha katika kila mchezo lazima kuwe na motisha kwa ajili ya wachezaji.

“Mfano katika michezo yetu iliyopita yote ya Ligi ya Mabingwa wachezaji wote walishapewa motisha zao kuanzia mchezo wa kwanza, hivyo wachezaji wapo salama na tupo tayari kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanacheza kwa kuipambania timu iweze kupata matokeo mazuri,” amesema kiongozi huyo

Naye Afisa Habari wa Young Africans, AIly Kamwe amesema kuwa: “Tunaamini kuwa mchezo bado haujaisha kama ambavyo watu wanaona kuwa mchezo umeisha kule Rwanda baada ya kushinda mabao 2-0.

“Nataka niwaambie kuwa kazi bado haijaisha na tayari tumewaambia wachezaji wetu kuwa tunatakiwa kupambana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa malengo yetu yanatimia ya kuipeleka timu kwenye hatua ya makundi Barani Afrika”

Waganda wapewa darasa Teknolojia mpya uchimbaji Madini
Robertinho: Nimesikia malalamiko ya Mashabiki