Timu za Saudi Arabia ikiwamo Al Nassr zimeanza kuwasiliana na wawakilishi wa beki wa kati wa Manchester United, Raphael Varane mwenye umri wa miaka 30, ili kuipata huduma yake dirisha lijalo la majira ya baridi.

Dirisha lililopita la usajili, jina la beki huyo kutoka nchini Ufaransa lilikuwa miongoni mwa mastaa waliosakwa kukipiga ligi Kuu ya Saudi Arabia lakini ilishindikana baada ya Man United kugoma kumuuza.

Al Nassr inaongoza kwenye harakati za kuinasa saini yake na hasa kutokana na nyota huyo kuwa na ukaribu na nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo waliocheza pamoja Real Madrid.

Beki huyo inadaiwa atawekewa mshahara wa Pauni 500,000 kwa juma ikiwa atasaini kwenye timu za Saudia.

Varane ambaye kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha ana mkataba wa kuendelea kusalia Man United hadi mwaka 2025, na anaonekana kuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa mashetani hao wekundu hali inayoonyesha huenda akapewa ofa ya kusaini mkataba mpya.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi tisa za michuano yote na majeraha ndiyo yamekuwa yakiathiri soka lake pale Old Tralford.

Namungo FC waisubiri Simba SC kwa hamu
Mfumo wa elimu ubadilishwe - Mdau wa Elimu