Taarifa kutoka nchini Syria zinasema kumekuwa na mpango wa makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya wapiganaji waasi na raia huko Daraya nje kidogo ya Damascus.

Hii imetokea tokea baada ya miaka mingi ya kuzingirwa na vikosi vinavyounga mkono serikali.

Serikali na mkuu mmoja wa makundi mawili wa waasi amesema wataanza kuondoka siku ya ijumaa.

Kituo cha Televisheni cha serikali kimetangaza kuwa raia wapatao elfu nne na wapiganaji mia saba wataruhusiwa kuondoka katika mji huo,Mji wa Daraya umezingirwa na vikosi vya serikali kuanzia mwaka 2012 kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara.

Temeke Yaandaa Operesheni Stendi Ya Mbagala
Watanzania Watakiwa Kumuenzi Baba Wa Taifa