Wapiganaji wa kundi la Mai-Mai wamemuua mwanajeshi mmoja wa Serikali walipovamia nyumba inayomilikiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na pande mbili, jeshi la Serikali na waasi hao, Rais Kabila hakuwa katika nyumba hiyo wakati wa shambulizi hilo.
Hata hivyo, wanajeshi wa Serikali walifanikiwa kuwadhibiti waasi hao na kuwafukuzia mbali na eneo hilo.
Hili ni tukio la pili la waasi kushambulia nyumba ya Kabila. Disemba mwaka jana, waasi walivamia nyumba ya rais Kabila iliyoko Kaskazini mwa jimbo la Kivu. Askari mmoja wa jeshi la polisi aliuawa katika shambulizi hilo.
- Tiffany awatolea uvivu wanaohangaika kujua aliyemng’ata Beyonce usoni
- Urusi yajibu mapigo ya Marekani, yawafukuza Wanadiplomasia 60
Hali ya usalama katika eneo hilo imeendelea kuwa tete kufuatia majaribio kadhaa ya makundi ya waasi nchini humo. Hali hiyo imechochewa na kitendo cha rais Kabila kukataa kuachia madaraka mwaka 2016 baada ya muda wake kuisha kikatiba.
Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu na tayari tume ya taifa ya uchaguzi imeshakabidhiwa sehemu kubwa ya bajeti kwa ajili ya kuanza maandalizi.