Serikali ya India imeidhinisha hukumu ya kifo, kwa wale watakaokutwa na hatia ya kuwabaka watoto wenye umri wa chini ya miaka 12.
Kulingana na ripoti ya shirika la habari la India Press Trust, baraza la mawaziri wa serikali ya Waziri mkuu Narendra Modi limepitisha amri hiyo na kuiwasilisha kwa rais ili aiidhinishe.
Aidha, Bunge la nchi hiyo litahitajika kuiidhinisha katika kipindi cha miezi sita ijayo amri hiyo ili iwe sheria. Lakini kwa sasa watuhumiwa wanaweza kushtakiwa chini ya amri hiyo.
Hata hivyo, hatua hiyo imejiri baada ya tukio lililozua ghadhabu hivi karibuni cha baada ya msichana mwenye umri wa miaka minane kubakwa na kuuawa katika jimbo la Jammu-Kashmir, pamoja na matukio mengine ya mashambulizi ya kingono dhidi ya watoto.
-
Democratic wamburuza mahakamani Trump na timu yake
-
Kijana aliyedukuwa mifumo ya FBI, CIA ahukumiwa
-
Korea Kaskazini yatangaza kuachana na makombora ya nyuklia