Mpango wa kuunda Mkoa mpya wa Chato umekumbwa na Changamoto ya kuendelea baada ya Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Kagera kukataa Maeneo ya Mkoa huo kuchukuliwa.

Hapo awali Kamati ya Ushauri ya ushauri ya mkoa wa Geita ilipendekeza baadhi ya maeneo ya wilaya za Geita, Kigoma na Kagera kuungana na kutengeneza Chato.

Maeneo hayo ni Bukombe na Chato (Geita), Biharamulo na Ngara (Kagera) na Kakonko ( Kigoma).

Wilaya ya Chato ilianzishwa mwaka 2007 ambapo katika uongozi wa Hayati Dk John Pombe Magufuli mpango wa kuifanya kuwa Mkoa ulianza na hivi karibuni katika kilele cha Kuzima Mwenge wa Uhuru huko Chato Rais Samia Suluhu Hassan alisema mipango inaendelea kuufanya mkoa.

Kesi ya Mbowe na wenzake kuendele leo shahidi awasili Mahakamani
Try Again: Kuna kitu hakipo sawa Simba SC