Mbunge wa Baraza la wawakilishi Louie Gohmert na wenzake wa Republican wamefungua kesi ya madai dhidi ya Makamu wa Rais Mike Pence ambaye ataongoza mkutano wa ujao wa Bunge utakaomilisha ushindi wa Rais mteule, Joe Biden.

Madai hayo ambayo Mwenyekiti wa chama cha Republican wa jimbo la Arizona, Kelly Ward na wenzake pia wamejiunga nayo, yataangalia uwezo wa Pence kama makamu wa Rais.

Sheria ya kuhesabu kura ya mwaka 1887 inasema Makamu wa Rais anapaswa kuongoza mkutano mkubwa wa Januari 6 wa Bunge kuhesabu kura za uchaguzi na kuhitimisha ushindi wa Biden dhidi ya Rais wa sasa, Donald Trump.

Madai hayo piabyanamtaka jaji wa mahakama ya Texas, Jeremy Kernodle, kumpa Pence mamlaka ya kipekee na uhuru pekee wa kuamua ni kura zipi za uchaguzi kutoka jimbo fulani zinapaswa kuhesabiwa.

Mlipili aibukia Kagera Sugar
Mwinyi: Tukioneana aibu hatutokwenda popote