Wabunge wa kambi ya upinzani katika Bunge la Kosovo wamefyatua gesi ya machozi bungeni wakati vikao vya bunge vikiendelea, kwa lengo la kuzuia bunge hilo kupitisha mkataba wasioupenda.
Wapinzani walifanya tukio hilo kama njia ya kuvuruga zoezi la upigaji kura kupitisha mkataba wa ujirani kuhusu mpaka kati ya nchi hiyo na Montenegro.
Kipande cha video kilichoonekana kwenye mitandao ya kijamii kinawaonesha wabunge wakitoka ndani ya bunge hilo wakiwa wanajifuta macho na kufunika pua zao kutokana na madhara ya gesi hiyo.
Kwa mujibu wa naibu spika wa bunge hilo, Avni Bytyci gesi hiyo ilifyatuliwa na mbunge wa upinzani, Levizja Vetvendosje.
“Mkataba wa mpaka kati yeu na Montenegro utapitishwa na bunge leo licha ya wabunge wachache wa upinzani kutaka kuvuruga kikao kwa kutumia njia ya vurugu,” alisema Bytyci.
- Msichana aliyewapiga makofi wanajeshi wenye bunduki afungwa jela
- Magazeti ya Tanzania leo Machi 22, 2018
Mkataba huo utawapa nafasi wananchi wa Kosovo kupata Visa bure ya kusafiri katika nchi za umoja wa Ulaya.