Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amejikuta katika wakati mgumu wakati wa kupitisha bajeti kuu ya Serikali mara baada ya kuzua hoja bungeni mjini Dodoma kuwa mbunge ambaye ataipinga bajetio hiyo hatastahili kupata mgawo huo.
Aidha, baadhi ya wabunge, wengi wao kutoka kambi ya upinzani waliokuwa wakionekana kuipinga bajeti hiyo, wamesema kuwa kwa hoja hiyo ya Spika haina lengo zuri kwa wananchi bali inataka kuligawa taifa.
Baada ya kumaliza zoezi la upiagaji kura, Ndugai alikaribisha miongozo ndipo mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi kunyanyuka na kuhoji kauli ya Spika wa bunge kama ilikuwa sahihi ama la, kitu ambacho kilizua mabishano makali bungeni kiasi cha kupelekea mbunge wa Ukonga, Isaya Mwita Chadema0) kutolewa nje.
Hata hivyo, Ndugai aliwaeleza mawaziri wakati wa upigaji kura ya upitishaji wa bajeti ya Serikali kuu kuwa mbunge atakayepiga kura ya hapana asipelekewe mgawo jimboni kwake kwakuwa hajakubaliana nayo.