Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema Ofisi hiyo itaendelea kutoa semina kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kuhusu tafsiri na dhana halisi kuhusu manufaa na faida za Biashara ya Kaboni ili kujenga uelewa wa pamoja katika jamii.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufunga semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Maji na Mazingira, Khamis amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha elimu kuhusu Biashara ya Kaboni inawafikia wabunge ambao wana ushawishi mkubwa kwa wananchi.

“Tumekusudia kutoa mafunzo haya kwa wabunge na wajumbe wa kamati zetu, mafunzo haya yanakuwa endelevu kwani sisi wabunge tuna ushawishi mkubwa katika jamii na tunalosema tunasikilizwa na wananchi” amesema Khamis.

Aidha, Khamis amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka maswali kutoka kwa wabunge na wananchi kwa ujumla kuhusu tafsiri na dhana halisi ya biashara hii huku wabunge wengi walipenda suala hili lipatiwe ufafanuzi wa Serikali kuhusu biashara ya kaboni, hivyo kwa kutambua umuhimu huo serikali imeandaa mpango wa mafunzo na semina mbalimbali kwa wabunge.

Azam FC, Singida BS kuanzisha timu za wanawake
Aliyejitoa ili mumewe apandishwe cheo kazini afunguka mazito