Waziri wa katiba na sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwasaidia kisheria wanawake waliotelekezwa na wanaume waliowazalisha ilipaswa kufanyika faragha na si kama ambavyo inaendeshwa kwa sasa.

Amesema hayo kufuatia swali lililoulizwa bungeni na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo.

Mbunge wa Geita vijijini, Joseph Msukuma amesema kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya.

Huku Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kampeni hiyo ni sahihi lakini kasoro yake ni kufanywa faragha.

Aidha Makonda ameweza kuainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kutokana na kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watoto kupatiwa bima ya Afya kwa ajili ya matibabu ya bure kwa kipindi cha mwaka mzima, lakini pia wababa kuitikia wito ambapo zaidi ya wababa 295 wamekubali kulea watoto wao, huku wengine 29 waomba kupimwa DNA kuthibitisha uhalali wa watoto wanaodaiwa kuwa ni kwao.

Na kampeni hiyo inatarajiwa kumalizika Aprili 20 mwaka huu kutokana na idadi kubwa ya wanawake waliojitokeza kusaidiwa kisheria.

 

EXCLUSIVE: Tazama Mabantu wakichambua mistari ya wimbo wa 'Sundi'
Picha: Alikiba afunga ndoa na binti wa Mombasa