Leo katika Mkutano wa 15 wa Bunge Jijini Dodoma wabunge wa upinzani wametoka nje ya bunge kupinga adhabu iliyotolewa kwa mbunge wa Kawe, Halima Mdee ambaye amesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwenye mikutano miwili ya bunge kuanzia leo.

Halima Mdee amepewa adhabu hiyo akidaiwa kuwa amelidharau Bunge kwa kuunga mkono hoja ya CAG iliyosema kuwa Bunge ni dhaifu.

Azimio hilo limewasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa kamati ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emanuel Mwakasaka amesema Mbunge huyo alipoitwa kwenya kamati ili kujieleza alikiri kutamka maneno hayo na kuonyesha kutojutia huku akidai kuwa ni maoni yake binafsi na anao uhuru wa kutoa maoni kama mwananchi.

Pia Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imethibitisha kutoshirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikal (CAG) Profesa Mussa Asadi kwa kudharau Bunge kwa kusema Bunge ni dhaifu na  hajutii na ataendelea kutumia neno hilo kwani kiuhasibu linamaanisha upungufu.

Aidha katika mikutano ya Bunge inayotarajiwa kufanyika wastani wa maswali 515 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na serikali na wastani wa maswali 88 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku ya alhamisi

Serikali yawaonya waliojipanga kuhujumu miradi
Polisi yamsaka 'Eric Holder' kwa udi na uvumba kuhusika kifo cha Nipsey