Mwenyekiti wa kamati ya HAMASA ya TAIFA STARS Haji Sunday Manara amewatia moyo wachezaji wa timu hiyo, huku akichukizwa na kebehi zinazendelea kutolewa na baadhi ya wadau wa soka kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa kundi D wa Fainali za Mataifa Bingwa ya Afrika dhidi ya Zambia.
Taifa Stars ilipoteza mchezo huo uliochezwa mjini Limbe Cameroon, kwa mabao mawili kwa sifuri, na kuipa nafasi Zambia kupata alama tatu muhimu kwenye msimamo wa kundi D.
Manara ameandika ujumbe huo, kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku akiwataka wachezaji kuamini wanaweza kumaliza michezo ya hatua ya makundi wakiwa na alama 6, ambazo zitaweza kuwavusha.
Manara ameandika: “Tanzania ina Rais mmoja lakini ina Makocha wajuaji Milioni kumi..
“Ina Waziri Mkuu mmoja lakini ina Wachambuzi wajuaji Milioni ishirini !!
Uzuri wa makocha na wachambuzi wetu hawajawahi kuongea lugha moja au inayofanana ktk kujua tunakwama wapi ?
Kila Mtanzania ni Mjuzi wa Soka Messi na Guardiola wanasubiri, wanaujua huu mchezo kuliko kamati nzima ya ufundi ya FIFA !!
Na ukitaka kuamini hilo wasome mitandaoni , kila mmoja wao atakueleza sababu tofauti za Kwa nn tulifungwa jana na Zambia,,
Yaani wajuzi hawa wa kitanzania huwa hawawi uniform hata Kwa asilimia kumi tu, kujua tunakwama wapi!!
Wenyewe always hutofautiana,
Kuna mmoja kaandika sababu ya kufungwa jana ni watangazaji wetu kufupisha jina la mchezaji wa Zambia Felix Kapumbu na kutumia jina la mwanzo tu la Felix.
Yes Hii ndio Tanzania yangu ambayo ujuaji wa soka upo juu kuliko Brazil au Germany..
Nakumbuka alipokuja Luis Figo baadhi ya wabongo wakawa wanamuelekeza Mwamba huyo misingi ya soka.
Kwenu wachezaji wetu wa Stars, mnaweza kupata points sita na mkavuka mlipo Insha’Allah.”
Taifa Stars itarejea tena dimbani Jumamosi (Januari 23) kucheza dhidi ya Namibia, kisha itamaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kupambana na Guinea ambao jana walianza vyema kwa kuichakaza Namibia mabao matatu kwa sifuri.