Raia wa Marekani wapo katika mkakati mkali wa kumuondoa Rais Donald Trump madarakani kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Ambapo kundi la waumini kutoka miji mikubwa ya Marekani wanaoamini nguvu za giza wamepanga kuungana Machi 26 mwaka huu kufanya tambiko kubwa na maalumu la kumuondoa Rais Donald Trump madarakani mapema iwezekanavyo.

Hatua hizo zimezua ghadhabu kutoka kwa waumini wa dini ya kikristo ambao wamewalalamikia wachawi hao kutangaza vita ya kiroho.

Pamoja na tambiko hilo kubwa na maalumu kutokea Machi 26, bado kuna matambiko mengine madogo madogo hufanyika kila siku kuhakikisha Trump anaondoka madarakani.

Wapinzani wengi wa Trump wanaamini kuwa itawapasa kusubiri kwa miaka minne ili waweze kumuondoa madarakani kwa kutumia sanduku la kura.

Hata hivyo wachawi hawakubaliani na Trump kukaa madarakani kwa mihula yote minne kwani matakwa yao ni kumuondoa Trump kabla muhula wake wa kwanza haujaisha.

Tangu jumuiya hiy0 ya wachawi kutangaza kuhusiana na tambiko hilo. Trump hajazungumzia lolote kuhusu tukio hilo.

 

Gianni Infantino: Afrika Ina Vipaji Vya Soka, Vinahitaji Kuendelezwa
MKwasa: Hali Ya Kifedha Sio Nzuri Young Africans