Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kinatarajia kuondoka jijini Dar es salaam leo jioni kuelekea Gaberone, Botswana tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya Kwanza.
Kikosi cha wachezaji 27 cha Simba SC na Maafisa wa Benchi la ufundi la klabu hiyo, kitaondoka jijini Dar es salaam kwa ndege maalum ya kukodi.
Orodha ya wachezaji watakaokua safarini imetolewa, ambapo Walinda Lango wataongozwa na Aishi Manula, Beno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salum.
Mabeki: Shomary Kapombe, Israel Mwenda, Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Kennedy Juma, Inonga Varane na Joash Onyango.
Viungo: Thadeo Lwanga, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajibu, Hassan Dilunga, Bernard Morrison, Peter Banda, Duncan Nyoni na Abdul Swamadu.
Washambuliaji: Meddie Kagere, John Boko na Kibu Denis
Simba SC itacheza dhidi ya Mabingwa wa Botswana Jwaneng Galaxy siku ya Jumapili (Oktoba 17), kisha itarejea jijini Dar es salaam kucheza mkondo wa pili Oktoba 22, Uwanja wa Benjamin Mkapa.