Baada ya kukubali kichapo cha mabao saba kwa sifuri kutoka kwa Mabingwa Watetezi Simba SC, imebainika kuwa hali si shwari ndani ya Coastal Union ya Tanga.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ya jijini Tanga umepanga kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya wachezaji wao, kufuatia kipigo hicho kitakatifu.

Coastal Union walikubali kipigo hicho ambacho ni kikubwa kutokea tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, huku uongozi ukisisitiza kipigo hicho kitokana na nidhamu mbovu ya wachezaji.

Madai ya nidhamu mbovu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, yemetolewa na mwenyekiti Coastal Union Steven Mguto, ambaye alikuwa shuhuda wa mpambano huo uliounguruma uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

“Tumeyakubali matokeo, ila tutaangalia cha kufanya kwenye hili, kuna wachezaji tutawachukulia hatua za kinidhamu,” amesema Mguto ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya ligi (TPLB).

Simba ambayo siku ya Ijumaa (Novemba 27) itakuwa ugenini kucheza mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau United imesema ushindi huo ni moja ya kipimo kizuri kwao kabla ya kuelekea Nigeria leo Jumanne Novemba 24.

Katika mchezo huo, Simba ilikuwa na mabadiliko machache, wakati mkongwe Erasto Nyoni akirejea kikosini kucheza nafasi ya Jonas Mkude na Bernard Morrison akianza na kufunga bao.

Said Ndemla aliendeleza kiwango chake bora tangu kuanza kupata nafasi katika kikosi cha Simba msimu huu, akiaminika kuichezesha timu na nahodha John Bocco akifunga hat trick ya pili kwenye Ligi Kuu msimu huu. Awali ilikuwa ya Adam Adam wa JKT Tanzania alipoifunga Mwadui FC.

Kocha Sven Vandenbroeck alisema ushindi huo mnono umekuwa chachu kwao na anaamini wataendelea na rekodi hiyo kwenye michezo ijazo ikiwamo ya Ligi ya mabingwa.

Nicolas Pepe aomba msamaha Arsenal
Simba SC safarini Nigeria

Comments

comments