Chama cha Soka nchini Italia, kimethibitisha kumfungia kiungo wa Juventus, Nicolo Fagioli, kujihusisha na soka kwa kipindi cha miezi saba kutokana na kukutwa na kosa la kujihusisha na masuala ya kubeti.
Mbali na kufungiwa huko, kiungo huyo wa Italia, pia amepigwa fainali ya euro 12,500.
Wakati huo huo, uchunguzi unaendelea kwa Sandro Tonali na Nicolò Zaniolo ambao wote ni raia wa Italia kutokana na kuhusishwa na michezo ya kubeti ambayo imekatazwa kwa wanasoka.
Fagioli amecheza mechi sita kati ya nane za Juventus katika Serie A msimu huu.
Novemba mwaka jana, alicheza mechi yake ya kwanza kwa Italia, akitokea benchi waliposhinda 3-1 dhidi ya Albania.
Tonali, ambaye amejiunga na Newcastle United msimu huu kutoka AC Milan, juzi Jumanne (Oktoba 17) alikutana na waendesha mashtaka mjini Turin, huku ikitajwa kwamba anaweza kupata adhabu kama Fagioli.